Mnyika: Wanataka ubunge kwa msilahi pekee

HomeKitaifa

Mnyika: Wanataka ubunge kwa msilahi pekee

Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika amefunguka na kusema kwamba baada ya Kamati Kuu kutoa uamuzi wao dhidi ya wanachama 19 walivuliwa uanachama wa chama hicho aliwafata na kuzungumza nao lakini alichogundua ni kuwa Mdee na wenzake wanataka kubaki bungeni kwa masilahi yao binafsi.

“Baada ya kutokea yaliyotokea nilikutana na Bulaya na wenzake ili dhamira yangu iniongoze sawa wamekosea,lakini je, wapo tayari kutubu na kurudi?

“Nilichogundua baada ya kufanya mazungumzo nao, mdomoni wanasema wanakipenda Chadema na wapo tayari kurudi na kushiriki kwenye chama, lakinituwaachie ubunge. Binafsi nilichokigundua kinachowaweka bungeni ni masilahi ya ubunge pekee, hakuna kingine,” alisema Mnyika.

Kifuatacho 

Mkurugenzi wa Mawasiliano Chadema, John Mrema alisema Baraza Kuu limekubaliana na uamuzi wa Kamati Kuu hivyo sasa utaratibu unaofuata ni Katibu wa Chama kupeleka barua bungeni.

“Hatua inayofuata ni Katibu Mkuu ataandika barua rasmi kwa Spika wa Bunge kumtaarifu uamuzi huo. Suala hili litakuwa mikononi mwa Spika, litakuwa limetoka mikononi mwa chama,

“Kwa sasa hawana tena nafasi ya kukataa rufaa, mamlaka ya rufaa yao ilikuwa mwisho Baraza Kuu kwa hiyo hawana ngazi nyingine ya kwenda. Kwa upande wa Chadema tumemalizana nalo hilo,” alisema Mrema.

error: Content is protected !!