Sekta ya Mawasiliano inazidi kukua nchini

HomeUncategorized

Sekta ya Mawasiliano inazidi kukua nchini

Kutokana na Hotuba ya Wazari wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, iliyosomwa na Waziri Nape Nnauye imeonesha kuwa Sekta ya Mawasiliano imeendelea kukua, huku takwimu zikionesha kuwa;

  1. Laini za simu zilizosajiliwa zimeongezeka kutoka milioni 55.7 Mwezi Aprili,2022 hadi kufikia milioni 62.3 mwezi Aprili,2023.
  2. Watumiaji wa intaneti wameongezeka kutoka milioni 29.9 Mwezi Aprili,2022 hadi milioni 33.1 Mwezi Aprili,2023.
  3. Watumiaji wa huduma za kutuma na kutoa pesa kwa njia ya mtandao wa simu wameongezeka kutoka milioni 35.7 mwezi Aprili,2022 hadi milioni 44.3 mwezi Aprili,2023.
  4. Watoa huduma wa huduma za ziada (Application Services and Value Added Services) wamefikia 141 ukilinganisha na watoa huduma 102 Mwezi Aprili, 2022 (ongezeko la asilimia 38).
  5. Watoa huduma wa Miundombinu ya Mawasiliano wamefikia 23 ukilinganisha na watoa huduma 22 Mwezi Aprili, 2022 (hii ni sawa na ongezeko la asilimia 4.5)

 

error: Content is protected !!