Ajinyonga kisa ujumbe wa ‘Tuma kwenye namba hii’

HomeKitaifa

Ajinyonga kisa ujumbe wa ‘Tuma kwenye namba hii’

Amos Tofiri (29), mkazi wa kijiji cha Lukunguni,mkoani Morogoro amejinyonga kutokana na deni la Sh 400,000 alizokopa na akazituma kwa mtu aliyemtumia ujumbe wa bandia katika simu ya mkononi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Fortunatus Muslimu alisema jana kwamba, Tofri alikopa fedha hizo baada ya mtu kumtumia ujumbe ameingizizwa Sh 400,000 na alitakiwa azirudishe kwa kuwa zilitumwa kimakosa.

Kamanda Muslimu alisema kijana huyo hakuchunguza ujumbe huyo, akaenda kwa wakala na kurudisha fedha hizo bila kuangalia salio katika simu yake na ndipo baadaye aligundua hakukuwa na ongezeko la fedha kwenye simu yake akaamua kujinyonga.

Tofri alijinyonga jirani na nyumba yao kwenye mti wa mfenesi kwa kutumia kamba ya katani na mwili wake uligunduliwa na mdogo wake, Ruti Tofri.

 

error: Content is protected !!