Harmonize aonesha kadi ya gari ya Kajala

HomeBurudani

Harmonize aonesha kadi ya gari ya Kajala

Baada ya kuwepo kwa maneno kuhusu gari alizonunua msanii Harmonize kwa ajili ya kumpa aliyewahi kuwa mpenzi wake, Kalaja Masanja ili aweze kumsamehe, Mmiliki huyo wa lebo ya Konde Gang ameweka hadharani kadi ya gari inayoonesha mmiliki halali wa gari ni Kajala.

Kadi ya gari yenye jina la Kajala kama mmiliki wa gari

Hivi karibuni Harmonize amenunua magari mawili aina ya Ranger Rover ambayo tayari yamepo nchi tayari kupelekwa kwa Kajala ambaya hajaonyesha dalili yoyote ya kupokea zawadi hizo kwani sio mara ya kwanza ananunuliwa vitu na msanii huyo.

Katika suala la kuomba msamaha, Harmonize alianza kwa kubandika picha yake akiwa na Kajala kwenye mataa ya Kinondoni, kununua zawadi kama maua ambayo hayakumfikia mlengwa, kutunga wimbo wa ‘YOU’ na sasa amenunua magari huku akiendelea kueleza hisia zake kwenye ukurasa wake wa Instagram.

error: Content is protected !!