Rais Samia aridhia waliovamia eneo la Uwanja wa KIA kulipwa fidia

HomeKitaifa

Rais Samia aridhia waliovamia eneo la Uwanja wa KIA kulipwa fidia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema serikali itawalipia fidia wale wote waliovamia eneo la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kilimanjaro (KIA) ili waweze kwenda kujenga sehemu nyingine.

Alisema hayo wakati akiwasalimia wananchi wa USA River mkoani Arusha leo Machi 5,2023.

“Serikali imekamilisha tathmini ya wale wote waliovamia pale pamoja na kwamba wamevamia, lakini serikali tumekubali kulipa fidia ili waachie lile eneo. Tathmini imeshafikishwa serikalini ni bilioni 11 serikali tunakwenda kulipa ili wale watu waachie lile eneo wakatafute makazi maeneo mengini,” amesema Rais Samia.

Aidha, Rais Samia amesema, serikali licha kwamba watu hao ni wavamizi lakini tayari walishajenga eneo hilo hivyo imeamua kuwalipa fidia ili waweze kwenda kuanzisha makazi mapya eneo lingine.

error: Content is protected !!