Rais Samia chanzo cha ongezeko la uwekezaji nchini

HomeKitaifa

Rais Samia chanzo cha ongezeko la uwekezaji nchini

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimetoa taarifa kuhusu mwenendo wa hali ya uwekezaji nchini katika kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Rais wa awamu ya sita, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na kueleza kwamba jumla ya miradi 575 imesajiliwa sawa na ongezeko la asilimia 26.

Taarifa ya TIC inaeleza kuwa ongezeko kubwa la miradi iliyosajiliwa linatokana na jitihada za Serikali za kutangaza fursa mbalimbali za Uwekezaji zilizoko nchini kupitia ziara za viongozi hasa Rais Samia pamoja na kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini.

Katika kipindi cha Awamu ya Sita, Machi 2021 hadi Feb 2023 ikilinganishwa kipindi kama hicho Machi 2019 hadi Feb 2021, thamani ya mitaji ya miradi ya uwekezaji iliyosajiliwa TIC imeongezeka kwa asilimia 173 kutoka Dola za Marekani 3.16 bilioni hadi Dola za Marekani 8.64 bilioni

TIC imefanikiwa kusajili jumla ya miradi 575 ambayo inakadiriwa kuwekeza kiasi cha mtaji wa Dola za Marekani bilioni 8,64 na kutoa jumla ya ajira 87,187.

Mchanganuo wa Kisekta wa Miradi iliyosajiliwa Machi 2021- Feb 2023

1.Kilimo – miradi 47 na kutoa ajira 9,133

2. Ujenzi/ Majengo ya Biashara- miradi 44 na kutoa ajira 4,452

3. Miundombinu- miradi 5 na kutoa ajira 17,233

4. Nishati- miradi 2 na kutoa ajira 95

5. Taasisi za kifedha- miradi 4 na kutoa ajira 2,869

6. Rasilimali Watu – miradi 17 na kutoa ajira 1,434

7. Viwanda- miradi 280 na kutoa ajira 44,664

8. Huduma- miradi 30 na kutoa ajira 2,479

9. Mawasiliano- miradi 2 na kutoa ajira 85

10. Utalii- miradi 48 na kutoa ajira 3,211

11. Usafirishaji- miradi 96 na kutoa ajira 1,532

Aidha, taarifa ya TIC imeeleza mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kuhamasisha Diplomasia ya Uchumi yamesaidia katika kuinua na kufanikisha uhamasishaji wa Uwekezaji nchini, kazi nzuri inayofanywa na Rais Samia kupitia ziara zake.

error: Content is protected !!