Willy Paul na Diana Marua wawashiana moto Kenya

HomeBurudani

Willy Paul na Diana Marua wawashiana moto Kenya

Msanii kutoka Kenya, Willy Paul ambaye miaka ya nyuma aliwahi kutamba na wimbo wake wa ‘Jigi Jigi’, ametupiana maneno kwenye mitandao ya kijamii na mrembo Diana Marua aliyewahi kuwa naye kwenye mahusiano lakini kwa sasa ni mke wa mwimbaji wa nyimbo za injili Bahati.

Vita hiyo ya Willy na Diana, imezua mshangao kwa wengi kwa kile alichosema Diana kwamba Willy Paul aliwahi kutaka kumbaka.

Hivi karibuni Willy Paul aliachia ngoma yake ambayo ndani yake anamuongelea mwanamke aliyewahi kuwa naye kwenye mahusiano na kumsema hivyo kupelekea watu kuhisi kwamba ni dhahiri wimbo huo amemuimbia Diana kwa sababu ndiye aliyekuwa naye hapo nyuma.

Diana naye akaweka video kwenye mtandao wa Youtube akilalamika na kulia huku akisema Willy Paul alishawahi kujaribu kumbaka na kuongezea kwamba wapo wasichana wengine wengi waliowahi kufanyiwa kitendo hicho na msanii huyo hivyo kumtuhumu kama mnyanyasaji wa wanawake.

Baada video hiyo watu wengi wamemlaumu na kumsema Willy Paul kwa kitendo hicho anachoshtumiwa kukifanya kwa Diana wakati wa mahusiano yao lakini pia nayeye hakukaa kimya, alijibu tuhuma hizo na kusema kwamba amesingiziwa kwani hakuwahi kufanya kitendo kama hicho.

“Mwambie mume wako ukweli, mwambie ulikuja kulala kwangu na nini kilitokea. Mimi sijawahi kumbaka mtu huo ni uongo mkubwa, na hapa juu ya jina la Mama yangu na watoto wangu, mueleze ukweli mume wako,” alisema Willy Paul.

Diana amesema kwamba anapeleka kesi mahakamani huku Willy Paul akisema kwamba aache uongo kwani mahusiano yao hayakuzidi hata masaa 24 hivyo aache kutafuta huruma kutoka kwa Wakenya pia ameomba vyombo vya usalama kuweza kumsaidia kukabiliana na mashtaka hayo dhidi yake.

error: Content is protected !!