Ruksa kumrekodi askari

HomeKitaifa

Ruksa kumrekodi askari

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Safia Jongo ametoa ruksa kwa abiria kuwarekodi kwa simu askari wa usalama barabarani wanaochukua rushwa kwa madereva na kisha kumtumia ili awashughulikie.

Kamanda Jongo amesema hayo leo wakati akizungumuza na madereva, abiria na mawakala wa vyombo vya usafiri kituo kikuu cha mabasi Geita katika uzinduzi wa wiki ya usalama barabarani.

Amesema imekuwa ni mazoea kwa maaskari wa usalama barabarani (trafiki) wanapokagua na kubaini gari lina mapungufu basi wanachukua pesa kwa madereva badala ya kuandika faini ama kuchukua hatua.

“Askari asipotekeleza wajibu wake, au askari akiwasimamisha, mkaona anachukua rushwa, rushwa, rushwa ni adui wa haki, rushwa ni chanzo cha ongezeko la ajali, tusikubali.” amesema Kamanda Jongo.

error: Content is protected !!