Njia 6 za kumpata mwanamke tajiri

HomeElimu

Njia 6 za kumpata mwanamke tajiri

Wanaume wengi wamekuwa waoga kumtongoza msichana ambaye amemzidi kipato au wengi huwaita wakishua na hii inawasababishia kushindwa kuwa na mtu sahihi katika mahusiano sababu ya uwoga.

Hizi hapa ni njia ambazo ukizitumia vyema basi lazima utaweza kuushinda moyo msichana yeyote tajiri.

Kuwa nadhifu

Sio tu wasichana matajiri bali kila msichana anapenda kuwa na mwanaume nadhifu, anayejipenda na kujijali.

Pangilia mavazi yako vizuri kuanzia juu mpaka chini kwenye viatu na pia kunukia kwani ukiwa hivi huwezi kukataliwa.

Ongea kwa akili

Wasichana wengi wakishua wanapenda mwanaume mwenye akili na ambaye ataweza kumpa ushauri wa kuendelea kimaisha hivyo kuwa sana makini pindi uongeapo na mwanamke wa aina hii.

Kwenye maongezi yako hakikisha haujisifu kwani kwa kufanya hivyo unaweza kujifukuzia ndege wako.

Chunguza anapenda nini

Hakikisha unachunguza na kujua anapenda vitu gani kisha na wewe uanze kupenda vitu hivyo ili muweze kwenda sawa.

Pia jihusishe na kufanya mambo anayopenda kama anapenda kukimbia basi na wewe anza kuwa mpenzi wa mbio.

Usiwe naye muda wote

Usiwe unawahi kupokea simu zake au kujibu haraka jumbe zake, kwani wasichana wa aina hii wanapenda mtu ambaye anafanya kazi muda wote na kujituma.

Endapo utakuwa unaongea naye muda wote na haoni kitu cha msingi unachifanya basi utaachwa kwenye mataa.

Kuwa mkweli

Usije ukajifanya una fedha nyingi ilimradi umridhishe mrembo huyo, kama hauna hakikisha anajua kwamba hauna kuliko kumdanganya. 

Unapokuwa mkweli kwake basi hata yeye atajua kwamba yupo na mtu sahihi na sio muongo.

Usilazimishe tendo la ndoa

Epuka kumlazisha kushiriki naye tendo la ndoa bali subiri mpaka yeye mwenyewe atakaporidhia kufanya hivyo.

error: Content is protected !!