Maombi kwa mapacha

HomeUncategorized

Maombi kwa mapacha

Hospitali ya Taifa Muhimbili inatarajia kufanya upasuaji mkubwa wa kutenganisha watoto pacha waliozaliwa wameungana sehemu ya kifua, tumbo na ini (lakini kila mtoto ana ini lake).

Kulingana na taarifa iliyotolewa na hospital hiyo, upasuaji huo unatarajiwa kufanyika Julai Mosi, 2022 kwa saa 6 hadi 7.

Tanzania itakuwa nchi ya tatu Barani Afrika kufanya upasuaji wa aina hii baada ya Afrika Kusini na Misri.

error: Content is protected !!