Rais Samia kumteua tena Mabeyo

HomeKitaifa

Rais Samia kumteua tena Mabeyo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameweka wazi kwamba CDF mstaafu Jenerali Venance Mabeyo, anataria kupangiwa kazi nyingine hivi karibuni.

“Lakini kama tulivyokwambia jana unaacha ukiwa kijana bado una nguvu na kwa maana hiyo tutaendelea kukuteua, tutaendelea kukupa majukumu uendelee kutusaidia nadhani jioni ya leo Katibu Mkuu kiongozi atasikia kwenye bomba tayari ameshakupangia kazi ya kufanya,” amesema Rais Samia.

Amesema hayo alipokuwa akitoa hotuba fupi wakati akiwaapisha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi mpya CDF John Jacob Mkunda na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania leo Tarehe 30 Juni,2022, Ikulu Dar es Salaam.

 

 

error: Content is protected !!