Serikali inavyowathamini wanaohamia Msomera

HomeKitaifa

Serikali inavyowathamini wanaohamia Msomera

Katika kuhakikisha wakazi wanaohama kutoka Ngorongoro wanakuwa na maisha bora zaidi katika makazi mapya Msomera, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameridhia kutoa motisha mbalimbali kwa wakazi hao.

Taarifa hiyo imetolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akitoa hoja ya kuahirisha mkutano wa saba wa bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo tarehe 30 Juni,2022.

Waziri Mkuu alisema imehakikisha kwamba kila kaya inayoondoka inapewa fidia ya nyumba aliyokuwa anaishi, nyumba zenye vyumba vitatu zilizojengwa kwenye eneo la ekari 2.5, godoro, tochi na ndoo.

Pia, kila kaya inapewa fedha za kutosha kwa ajili ya kuanzia maisha kwenye makazi mapya.

Kila kaya inapewa mahindi magunia mawili kwa kipindi cha miezi mitatu kwa ajili ya kujikimu katika kipindi cha mpito wakati wakazi wakijiandaa na maandalizi ya kilimo.

Na pia, kila kaya inapewa shamba lenye ukubwa wa ekari tano na zitakabidhiwa hati za kumiliki ardhi kwa ajili ya eneo la nyumba

Waziri Mkuu pia amewataka viongozi na watendaji kuendelea kuelimisha, kuhamasisha na kuwashirikisha wananchi na wadau wengine hususan wenyeji katika utekelezaji wa zoezi hilo.

error: Content is protected !!