67.2% ya wakazi wa Dar wana uzito uliopitiliza

HomeKitaifa

67.2% ya wakazi wa Dar wana uzito uliopitiliza

Utafiti wa hivi karibuni umeonyesha kwamba asilimia 67.2 ya wakazi wa Dar es Salaam wana uzito kupita kiasi huku wengi wao wakiwa ni wanywaji wa pombe wa mara kwa mara.

Dk Pedro Pallangyo, Mkuu wa Idara ya Utafiti na Mafunzo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) amesema utafiti huo ulifanyika mwaka 2020 ukihusisha watu 6,691 ni utafiti mkubwa zaidi kuwahi kufanyika nchini, ulihisisha wanawake na wanaume.

“Tuliangalia aina ya ulaji wa watu, ufanyaji wa mazoezi, unywaji wa maji na uvutajai wa sigara,

“Kikubwa ni kwamba wanakula si kwa sababu wanakosa mlo, ila kwa sababu hawana nidhamu ya muda wa kula, wanakula chakula ambacho si kizuri kiafya,” alisema.

Aliwataja wenye shinikizo la juu la damu, wanaywaji wa pombe na watu wasiozingatia unywaji maji kuingia kwenye hatari hiyo ya uzito uliokithiri kulingana na utafiti huo.

Kuhusu ufanyaji wa mazoezi, Dk Pedro alisema asilimia 88.3 ya watu wote waliofanyiwa utafiti hawakuwa na tabia ya kushughulisha mwili walau nusu saa kwa siku tano kwa wiki.

Alisema mapendekezo ya WHO yameelekeza mtu kufanya mazoezi kwa saa mbili na nusu kwa siku tano kwa wiki.

error: Content is protected !!