Vinywaji vinavyopunguza maji mwilini

HomeElimu

Vinywaji vinavyopunguza maji mwilini

Kwa kawaida tunakunywa maji mengi na vimiminika kwa wingi ili kuongeza maji mwilini lakini sivinywaji vyote huongeza maji mwilini kwani vingine husababisha kupungua kwa maji mwilini (dehydration).

Pombe
haijalishi hii ni mvinyo, pombe kali, bia na kinywaji kingine chochote chenye pombe ndani yake. Unapozidi kunywa hata kama ni kidogo, ndivyo unavyozidi kwenda chooni na kupoteza maji mengi zaidi ya kiasi cha pombe uliyokunywa.

Soda na sharubati
Kunywa soda baridi kipindi cha joto kali husaidia kujisikia nafuu lakini pia humaliza maji mwilini. Vinywaji vya sukari huongeza kiu na kuongeza glukosi kwenye damu ambayo hupelekea mwili kutumia maji mengi kusawazisha glukosi huku ubongo ukipokea ujumbe kuwa mwili hauna maji ya kutosha.

Kunywa sharubati kwa kiasi na ikiwezekana kunywa zaidi juisi za kutengeneza kwa matunda nyumbani “Fresh juice”.

Kahawa
Kahawa ina kafeini ambayo mbali na kukuchangamsha uinywapo sana hupelekea mwili kukosa maji ya kutoshahata kuongeza njaa hivyo kabala hujanywa kahawa hakikisha unakunywa maji ya kutosha na kuendelea kunywa maji hata baada ya kunywa kahawa au kinywaji chochote chenye kafeini.

Vinywaji vya kuongeza nguvu (energy drinks)
Vinywaji hivi vina sukari na kafeini nyingi pamoja na kemikali nyingine nyingi zinazoenda kukufanya uchoke mapema kama hautakunywa na maji mengi. Hupelekea kupoteza maji mwilini na hata midomo kupasuka mbali na madhara mengine mengi yatokanayo na vinywaji hivi.

error: Content is protected !!