Rais Samia : Punguzeni kidogo spidi

HomeKitaifa

Rais Samia : Punguzeni kidogo spidi

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi Runzewe Wilaya ya Bukombe mkoani Geita kupunguza kasi ya kuzaa ili huduma za kijamii na fursa za maendeleo zilizoko zitokesheleze katika kuboresha maisha ya kila Mtanzania.

Kauli hiyo ilikuja baada ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Shaka Hamdu Shaka kuwataka wananchi wa eneo hilo kuendelea kuzaa kwa kuwa huduma za kijamii zinaendelea kuboreshwa.

“Sasa mnakata nini? Zaeni tu mama yupo, madarasa yanajengwa, zaeni tu vituo vya afya vinajengwa, zaeni tu mama amefungua frusa , wawekezaji wanakuja,” alisema Shaka.

Baada ya Shaka kumaliza kuzungumza, Rais Samia alisema “ Mheshimiwa hilo la zaeni tu hapana bwana, jana (juzi) nilisimama Buseresere, ninaambiwa kituo kiomja kinazalisha watoto 1,000 kwa mwezi, sasa hapo baada ya miaka miatatu ni madarasa mnagapi? Kama ni vituo vya afya vingapi, tani za chakula ngapi? Punguzeni kidogo speed (kasi).”

Rais Samia akiwa mkoani Kigoma, alifungua miradi ya maendeleo ikiwamo Hospitalu ya Wilaya ya Kakonko ikigharimu zaidi ya Sh. bilioni 3.5, alifungua pia Kituo cha njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa KV 220 wenye urefu wa kilimota 144 kilichopo Nyakanazi na kufungua barabara ya Nyakanazi- Kabingo yenye urefu wa kilometa 50 iliyogharimu Sh. bilioni 43.

error: Content is protected !!