Rais Samia aipongeza Yanga SC

HomeMichezo

Rais Samia aipongeza Yanga SC

Rais wa Samia Suluhu Hassan, ameipongeza Yanga SC, kwa kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, baada ya kuishushia kichapo cha mabao 4-0 CR Belouizadad jana Jumamosi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rais Samia ameandika “Naipongeza Klabu ya Yanga kwa kufanya vyema katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), na kufanikiwa kufuzu hatua ya Robo Fainali. Mafanikio haya yameandika historia kubwa kwa klabu na sekta ya michezo nchini. Mmeleta furaha kwa mamilioni ya mashabiki wenu na Watanzania kwa ujumla”

 

error: Content is protected !!