SGR yaanza majaribio leo Dar hadi Morogoro

HomeKitaifa

SGR yaanza majaribio leo Dar hadi Morogoro

Shirika la Reli Tanzania (TRC) leo February 26,2024 limeanza safari yake ya kwanza rasmi ya majaribio ya treni ya SGR kutoka Dar es salaam hadi Mkoani Morogoro, hii ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye aliagiza hadi kufikia July mwaka huu safari za SGR kutoka Dar hadi Dodoma ziwe zimeanza.

Itakumbukwa Rais Samia wakati akitoa salamu za mwaka mpya kwa Taifa December 31,2023 pamoja na mambo mengine kupitia hotuba yake aliagiza hadi kufikia mwisho wa mwezi July mwaka huu 2024 safari za treni kupitia reli ya SGR kutoka Dar es salaam kwenda Dodoma ziwe zimeanza.

Rais Samia alinukuliwa akisema “Nimekuwa nikisikia mabadiliko ya tarehe za kuanza kwa safari za treni kupitia reli ya SGR kutoka Dar es salaam kwenda Dodoma na kwakweli Wananchi wamechoshwa na vijisababu wanataka kuona reli ikifanya kazi, sasa naelekeza ifikapo mwisho wa mwezi July 2024 safari ya reli ya SGR kati ya Dar es salaam hadi Dodoma ziwe zimeanza”

 

error: Content is protected !!