Rekodi yavunjwa ongezeko la watalii wa kigeni

HomeKitaifa

Rekodi yavunjwa ongezeko la watalii wa kigeni

Mapato yanayotokana na utalii yamezidi kuongezeka kutoka Dola za Kimarekani bilioni 1.3 mwaka 2021 hadi kuvunja rekodi na kufikia Dola za Kimarekani bilioni 3.37 ( takribani TZS Trilioni 8) mwaka 2023.

Taarifa ya ongezeko hili imetolewa na Ripoti mpya ya Benki Kuu ya funga mwaka 2023 katika sekta mbalimbali iliyotolewa Februari 16,2024 imefananua mafanikio hayo ya sekta ya utalii.

Ripoti hiyo imeonyesha pia ongezeko katika idadi ya watalii wa kigeni ambapo sasa idadi ya watalii wa kigeni walioingia ni milioni 1.8 idadi ambayo haijawahi kufikiwa tangu nchi ipate uhuru.

Jitihada zilizofanywa na Rais Samia Suluhu katika kutangaza vivutio vya kitalii vilivyopo nchini vimefanikisha ongezeko hilo la mapato na watalii nchini.

error: Content is protected !!