Tetesi za Soka Ulaya leo Oktoba 21 (Tielemans mbioni kuikacha Leicester City, huku Dyabala mambo safi ndani ya Juventus)

HomeMichezo

Tetesi za Soka Ulaya leo Oktoba 21 (Tielemans mbioni kuikacha Leicester City, huku Dyabala mambo safi ndani ya Juventus)

Kiungo wa Leicester City Youri Tielemans 24, amekataa ofa ya kuongeza mkataba mpya, na kuvifanya vilabu vya Manchester United, Chelsea, Liverpool, Real Madrid, Atletico Madrid na Bayern Munich kukaa mguu sawa (90 mins). Kiungo huyu ambaye yupo kwenye kiwango cha hali juu msimu huu anahitaji kutoka Leicester kwenda klabu nyingine kukabili changamoto mpya.

Manchester City wanamsaka mshambuliaji wa Fiorentina, Dusan Vlahovic, 21 (Tuttosport via Manchester Evening News). City wamekuwa wakimfuatilia mchezaji huyu bila kukata tamaa, endapo watafanikiwa kupta saini ya mchezaji huyu ataisaidi safu ya ushambuliaji kuwa imara zaidi.

Mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala 27, yupo hatua za mwisho kusaini mkataba mpya na vigogo wa Italia Juventus, makamu wa rais wa klabu hiyo Pavel Nedved amethibitisha (Football Italia)

Klabu Chelsea bado haijakata tamaa ya kumsajili mshambuliaji wa Borrusia Dortmund, Erling Haaland 21, kocha Thomas Tuchel anasema bado wanaangalia uwezekano wa kumpata mchezaji huyo (Bild via The Sun).

> Tetesi za Soka Ulaya  Oktoba 17, 2021

Klabu za Manchester City na mahasimu wao Manchester United vinafikiria kuchuana na Barcelona katika mbio za kusaka saini ya mshambuliaji wa RB Leipzig na Hispania Dani Olmo (Christian Falk on Twitter).

Wamiliki wapya wa Newcastle United bado hawajafikia maamuzi ya mwisho kuhusu kocha wa kumuajiri, huku kocha wa timu ya taifa ya Ubelgiji Roberto Martinez, aliyekuwa kocha wa Chelsea Frank Lampard, Lucien Favre, kocha wa Rangers Steven Gerrard na aliyekuwa kocha wa Bournemouth Eddie Howe bado wanaendelea kufuatiliwa (Guardian).

Tottenham imejiunga katika orodha ndefu ya vilabu ikiwemo West Ham -ya ligi kuu England kumfuatilia mshambuliaji wa Genk Paul Onuachu. Klabu yake hiyo ya Ubelgiji inataka ada ya £20m ili kumuachia Mnigeria huyo (Daily Mail).

Brighton wanamfuatilia mshambuliaji wa Clermont raia wa Guinea, Mohamed Bayo 23, ambaye klabu yake hiyo ya Ufaransa inataka ada ya £10m, Bayo amekuwa akifananaishwa na mshambuliaji wa Chelsea Romelu Lukaku (Argus).

Bruno Fernandes 27, alitishia kuondoka baada ya kusikia klabu yake ya Manchester United ilikua moja ya vilabu 12 vilivyosaini mpango wa kuanzishwa kwa ligi mpya ya Ulaya “European Super League (The Athletic).

error: Content is protected !!