Tetesi za Soka Ulaya leo Oktoba 17, 2021 (Ansu Fati bado yupo sana Barcelona, Newcaste na Leeds zamkosa Joe Rothwell)

HomeMichezo

Tetesi za Soka Ulaya leo Oktoba 17, 2021 (Ansu Fati bado yupo sana Barcelona, Newcaste na Leeds zamkosa Joe Rothwell)

Mshanbuliaji wa Barcelona Ansu Fati 18, amekubali kusaini mkataba mpya wa muda mrefu kusalia Barcelona kukiwa na kipengele cha ada ya £846m, akitaka kuondoka kama ilivyo kwa nyota mwenzake wa Hispania Pedri, 18 (Fabrizio Romano via Twitter).

Wamiliki wapya wa Newcastle hawajazungumza bado na kocha Steve Bruce baada timu hiyokuchapwa na Tottenham Hotspurs Jumapili (Daily Star).

Beki wa Atletico Madrid na England Kieran Trippier 31, ambaye alikua akihusishwa sana na mipango ya kuhamia Manchester United msimu uliopita, anasema angelipenda kucheza ligi kuu ya England kwa mara nyingine (Mirror).

Klabu ya Aston Villa itapaswa kuharakisha kumsaini nyota wa River Plate Julian Alvarez kwakuwa klabu ya ligi kuu Italia (Serie A) ya AC Milan wanamtaka pia mshambuliaji huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 21 (Calciomercato – Italia)

> Tetesi za Soka Ulaya  Oktoba 19, 2021

Beki wa Uholanzi Matthijs de Ligt 22, hana furaha Juventus, hali inayomsukuma wakala wake Mino Raiola kufanya mazungumzo na Barcelona kuhusu uwezekano wa kuhamia huko (Sport – Spanish).

Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer ana mpango wa kuwaachia wachezaji watano dirisha dogo la Januari litakapofunguliwa (Sun).

Klabu za Newcastle United Leeds United zitamkosa kiungo wa Blackburn Rovers Joe Rothwell (26) baada ya nyota huyo kuamua kusaini klabu ya Rangers (TEAMtalk).

Klabu za Liverpool, Borussia Dortmund au RB Leipzig zitapaswa kulipa kati ya euro milioni 30 – 40 kupata saini ya mshambuliaji wa RB Salzburg Karim Adeyemi, 19 (ORF – German).

Mshambuliaji wa FC Dallas na Marekani Ricardo Pepi (18) ameviweka roho juu vilabu vikubwa Ulaya ikiwemo Liverpool na Bayern Munich baada ya kuomba kuondoka rasmi klabuni hapo, lakini mchezaji huyo ameshakubaliana malipo binafsi na mshahara na klabu Wolfsburg (CBS Sport).

error: Content is protected !!