Moto masokoni tangu 2021-2022

HomeKitaifa

Moto masokoni tangu 2021-2022

Leo Aprili 8,2022 tukio jipya la moto limeripotiwa ambapo sehemu ya soko la Karume limetekea na moto. Matukio haya ya moto yameonekana kuongezeka hivi karibuni katika masoko na maeneo ya wafanyabiashara wadogo.

Yafuatayo ni baadhi ya matukio ya moto yaliyoripotiwa kwa kipindi kuaniza 2021 hadi Aprili 8, 2022.

Julai 10,2021

Soko kuu la Kariakoo jijini Dar es Salaam linalohudumia wafanyabiashara kutoka maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi liliteketea kwa moto huku zaidi ya maduka 200 yakiripotiwa kuungua.

Oktoba 19,2021

Soko la uyole jijini Mbeya ambalo linatumiwa na wafanyabiashara wadogo takribani 220 liliteketea kwa moto.

Oktoba 26,2021

Moto ambao chake hakikufahamika uliteketeza baadhi ya vibanda katika Soko la Mashine Tatu, mkoani Iringa.

Novemba 12,2021

Vibanda vya wafanyabiashara wadogo eneo la Mabibo Hostel, barabara ya Mandela jijni Dar es Salaam viliteketezwa kwa moto huku chanzo chake kikiwa hakijafahamika.

Novemba 14,2021

Vibanda vya wafanyabiashara wadogo eneo la Mwenge, Barabara ya Coca-Cola jijini Dar es Salaam viliteketea kwa moto ambao uliweza kudhibitiwa na Jeshi la Zimamoto.

Novemba 16,2021

Maduka zaidi ya 43 katika soko maarufu kwa biashara ya nguo, vipodozi na vifaa vya magari huko Tunduma, mkoani Songwe, linalofahamika kama Soko la Manzese liliteketea kwa moto.

Novemba 20,2021

Vibanda na maduka ya wafanyabiashara katika Soko la CCM Katoro, wilaya ya Geita viliungua na moto ambao chanzo chake hakikufahamika.

Disemba 15,2021

Vibanda zaidi ya 10 vya wafanyabiashara katika Soko la Sabasaba jijini Dodoma vyateketea kwa moto. Chanzo kikiwa ni uchomaji ovyo wa taka unaofanywa.

Januari 16,2022

Soko la Karume jijini Dar es Salaam maarufu kwa biashara ya mitumba linalotumiwa na wafanyabiashara zaidi ya 3500 lateketea kwa moto. Moto huo unatajwa kuteketeza asilimia 98 ya vitu vilivyokuwepo eneo hilo licha ya jitihada za wananchi na mamlaka husikia kupambana kuuzima.

Februari 1,2022

Soko la Mbuyuni, wilayani Moshi, mkoani Kilimanjaro lateketea kwa moto kabla ya vikosi vya polisi na Jeshi la Zimamoto, kwa kushurikiana na raia kuzima moto huo ambao chanzo chake hakikufahamika.

Aprili 8,2022

Soko la Karume lililopo Ilala jijini Dar es Salaam limeteketea kwa moto kwa mara nyingine alfajiri ya leo Aprili 8,2022. Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana.

error: Content is protected !!