Watumishi na viongozi wa Serikali washiriki kulima bangi Kilosa

HomeKitaifa

Watumishi na viongozi wa Serikali washiriki kulima bangi Kilosa

Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Alhaji Majid Mwanga amewataja baadhi ya viongozi, watumishi wa umma wa vijiji, vitongoji na kata zinazozunguka msitu wa Mkwiva uliopo wilayani kujihusisha na kilimo cha bangi na uharibifu ndani ya msitu huo.

“Tumetembelea msitu wa Mkwiva, kusema kweli kinachofanyika kule ndani ni uharibifu mkubwa. Wananchi, viongozi na watumishi wa umma wameshiriki kuharibu, ambapo baadhi yao wanalima bangi, mazao mengine, wanaruhusu mifugo hali ambayo imesababisha vyanzo vya maji kukauka,” alisema Mwanga.

> Polisi wakamata bangi ndani ya gereza

Mkuu huyo wa Wilaya alisema Serikali inamshikilia Mtendaji wa Kijiji na wananchi wawili ambao wanahusika na mashamba hayo huku Mwenyekiti wa Kijiji akiwa nje kwa dhamana na kutoa onyo kwa yeyote ambaye atabainika kulima bangi hatua kali bila kuangalia nafasi yake itachukuliwa dhidi yake.

Pia alitoa maagizo kwa TFS kuhakikisha hali ya msitu wa Mkwiva inarejea katika hali yake, watu wote ambao wanahusika na uharibifu wachukuliwe hatua haraka iwezekananvyo.

error: Content is protected !!