Kamera za usalama kufungwa nchini

HomeKitaifa

Kamera za usalama kufungwa nchini

Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa, ameagiza Wizara ya Teknolojia ya Habari kushirikiana na Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi kufunga kamera za ulinzi kwenye maeneo muhimu ya mkakati ikiwamo miji na majiji ili kudhibiti matukio ya uhalifu.

Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa Tano wa Tehama uliofanyika jijini Arusha Oktoba 20,2021 Waziri Mkuu Majaliwa aliipongeza Zanzibar kwa kuanza kufunga kamera hizo ili kudhibiti uhalifu katika maeneo mbalimbali na kusisitiza wizara hizo zinapaswa kukaa pamoj ili kuainisha jiji moja litakalotumikaa kama mfano kati ya miji na majiji itakayoanza kufunga kamera hizo.

  > Mambo 6 yaliyozungumzwa na Marais wa Tanzania na Burundi

Pia kwa mujibu wa Ripoti ya tathimini ya usalama duniani ya mwaka 2020 iliyoratibiwa na Shirika la Mawasiliano Duniani (ITU), Tanzania imeshika nafasi ya pili kwa Afrika katika ubora na ukomavu wa usalama wa mtandaoni.

Waziri Mkuu pia ameagiza Wizara ya Habari kuwasilisha ofisini kwake kila mwaka kupitia kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) mapendekezo ya vivutio vya uwekezaji katika sekta ya TEHAMA pia Tume ya TEHAMA kuweka mikakati mahsusi ya kusajili wataalamu wa TEHAMA ili kufikia lengo la usajili kutoka 700 hadi kufikia 5,000 mwaka wa 2025.

error: Content is protected !!