Aina 5 za wanaume wanaoweza kuathiri mafanikio yako

HomeElimu

Aina 5 za wanaume wanaoweza kuathiri mafanikio yako

Wanasema aina ya watu wanaokuzunguka inaweza kuonesha aina ya maisha unayoishi ama unayotamani kuyaishi. Huwezi kupenda mafanikio nauzungukwe na watu wasiopenda mafanikio, kwa namna moja au nyingine watajaribu kukuvuta na wewe uyaone mafanikio kwa jicho lao.

Inapokuja kwenye mahusiano kuna aina mbalimbali za wakaka, ni vyema kujua mapema wewe upo kundi gani na nini ufanye ama mpenzi wako ni kundi gani na kama anafaa kwa aina ya maisha unayoyataka.

Mlalamishi
Huyu anatumia saa nyingi kulalamika juu ya maisha kuwa magumu, atalalama kuhusu matatizo yake ya jana, juzi na siku nyingine zote za nyuma. Ni ngumu kwake kufanikiwa kwani muda nwingi anatazama yaliyopita zaidi ya yajayo na nini afanye kwaajili ya kesho yake. utamsikia akisema kwanini mimi …, mbona yule… kwanini wao…

Mwenye wasiwasi
Huyu yeye jana yake haimpi shida, kwanza hana habari nayo. Anaiwaza kesho yake na kujawa hofu kiasi cha kushindwa kutenda aliyopanga kuyafanya akiogopa kushindwa ama kuchekwa. Yeye huwaza maswali mengi ya vipi kama nitashindwa? je isipotokea itakuwaje?

Mwenye Subira
Moja kati ya vitu vya kuzingatia kwa mpenzi wako awe ni mtu mwenye subira na mvumilivu. Ukiwa na huyu yeye atakutuliza hata kwenye dhoruba kali. Tatizo ni kwamba ameridhika na hali aliyonayo na haoni sababu ya kuibadili hali hiyo. Yeye anangoja nguvu za Mungu zitende miujiza kwenye maisha yake bila yeye kujigusa.

Huyu anajua mahusiano yake yana tatizo, analijua tatizo lakini hayupo tayari kutatua changamoto hizo anaziangalia kama hazipo kabisa. anataka uhusiano mzuri na watoto wake lakini hawezi kutenga muda kukaa nao.

Aliyejeruhiwa
Yeye analia moyoni. Matatizo yake yote anayapokea na kukaa nayo yeye kimya. anabeba maumivu ya nyuma na ya sasa na anajua anaumia ila yupo tayari kuishi na maumivu hayo. Huyu anaweza kuwa na hasira sana, mbinafsi au hana ujasii kabisa.

Atakuaminisha kuwa anajipenda huku pia akijaribu kukufanya uone yeye ni bora kuliko wewe ili tu aweze kujiamini akiwa na wewe. Hii inaweza kupelekea wewe kuwaza kama upo sahihi au la.

Shujaa
Huyu halalami, hana wasiwasi, ana subira yenye kiasi, na anajua majeraha yake na anajitahidi kuachana nayo. Huyu hasubiri muujiza pekee lakini anachapa kazi, anajitahidi kuacha ya nyuma yabaki nyuma na kupambana awe na kesho nzuri zaidi.

Tofauti na aliyejeruhiwa huyu haogopi majeraha hivyo kila siku huamka akiwa na hamasa ya kujaribu tena ili aache historia nzuri na atimize malengo yake.

Je? mwanaume wako ama rafiki yako wa kiume wa karibu yupo kundi gani? Na wamshauri afanye nini?

error: Content is protected !!