Mambo 3 aliyofanya Rais Samia kwa wanafunzi wa vyuo

HomeElimu

Mambo 3 aliyofanya Rais Samia kwa wanafunzi wa vyuo

Mwaka mmoja sasa tangu Rais Samia Suluhu Hassan atimize mwaka mmoja madarakani ambapo amejitahidi kuhakikisha anagusa maisha ya Watanzania wengi kwenye sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya elimu.

Kwa wanafunzi wa elimu ya msingi na sekondari uongozi wa Rais Samia umefanikiwa kuongeza madarasa, madawati na vifaa vya kujifunzia bila kuwasahau wanafunzi wanaopata elimu katika vyuo mbalimbali nchini.

Kuongeza mkopo kwa asilimia 22.8
Mkopo kwa wanachuo umeongezeka kwa 22.8% sawa na TSZ 106 bilionifunzi wengi zaidi kuongezeka kwenye list ya wale wanaopokea mkopo na kupunguza vilio vya wanafunzi wengi ambao hushindwa kushiriki kikamilifu kwenye masomo yao.

Kwa mara ya kwanza HESLB imepata kiwango cha fedha nyingi zaidi kwenye bajeti ya 2021/ 2022 ya ZS 570 bilioni uliowanufaisha wanafunzi 160,000.

Kutolewa kwa ada ya uhifadhi mkopo “retention fee”
Unapopata mkopo kutoka Bodi ya Mkopo wa Elimu ya Juu (HESLB) unaporejesha hupaswa kurejesha na ‘retention fee’ ambayo ni 6% ya mkopo wa mdeni. Alipoingia Rais Samia madarakani alimtua mwanafunzi mzigo huo na kuondoa gharama hiyo kama sehemu ya marejesho.

Kuongeza umri wa tegemezi kwenye bima za afya
Moja kati ya vitu vya lazima kuwa navyo kabla ya kuanza masomo chuoni ni pamoja na kukata bima ya afya.

Awali tegemezi alipaswa kuwa na miaka isiyozidi 18 hivyo kufanya wanachuo ambao wengi wao wana umri wa juu ya miaka 18. Lakini Rais Samia aliamuru kubadilishwa kwa kifungu hicho na umri wa tegemezi kuwa miaka 21, agizo ambalo limeshatekelezwa na NHIF pamoja na Bunge kupitisha mswada huo.

Serikali ipo mbioni kuwa na chuo cha VETA Dodoma kitakachokua na uwezo wa kuchukua wanafunzi takribani 3000.

error: Content is protected !!