Waliomuua AKA wakamatwa

HomeKimataifa

Waliomuua AKA wakamatwa

Polisi wa South Africa wamethibitisha kuwakamata Washukiwa sita wa mauaji ya Rapper Kiernan Forbes maarufu AKA na kusema miongoni mwao ni ‘Mastermind’ aliyeandaa mpango mzima na kulipa wote Wauaji wote walioshiriki tukio hilo la February 10 2023.

Waziri anayehusika na Idara ya Polisi Bheki Cele amesema Watu hao sita watafikishwa Mahakamani Alhamisi hii February 29 ambapo mwenye umri mkubwa kati yao ana miaka 36, wa kwanza ni huyo Muandaaji Mkuu ‘Mastermind’, Watumia bunduki wawili, watoa taarifa wawili na mmoja wa mwisho ni aliyehusika kutafuta silaha na magari.

Waziri Cele amesema miongoni mwa waliokamatwa wamewahi kuhusishwa na mauaji ya kutisha ambapo walikimbilia Nchi jirani ya Eswatini ( zamani Swaziland) kujificha lakini tayari wamekamatwa na taratibu za kuwarejesha South Africa zilishaanza kufanyiwa kazi.

Pamoja na kwamba Polisi wamesema hawatozungumzia nia ya mauaji hayo, imefahamika kwamba Wauaji walianza kumfuatilia AKA kuanzia anawasili uwanja wa Ndege wa Durban hadi kwenye Mgahawa alikouawa.

South Africa ni moja ya Nchi zinazotajwa kuwa na mauaji mengi ya risasi yanayohusu visa vya kimaisha na wizi ambapo AKA sio Staa wa kwanza kuuawa kwa risasi kwani mwaka 2007 Staa wa muziki wa reggae Lucky Dube aliuawa kwa kupigwa risasi tatu na Majambazi baada ya kushindikana kwa jaribio la kumuibia gari lake ( Chrysler 300c) wakati akishusha Watoto wake kwa Ndugu.

Unaambiwa kwa mujibu wa rekodi zilizotolewa na Polisi mwezi uliopita, Taifa hilo lenye Mafundi wa amapiano lilirekodi vifo karibu 84 kila siku kuanzia October hadi December 2023.

error: Content is protected !!