Tetesi za Soka Ulaya leo Oktoba 27 (Benitez mbioni kurudi Newcastle, huku Chelsea wakipata fursa ya kumsajili de Ligt)

HomeMichezo

Tetesi za Soka Ulaya leo Oktoba 27 (Benitez mbioni kurudi Newcastle, huku Chelsea wakipata fursa ya kumsajili de Ligt)

Klabu ya Newcastle United haijakata tamaa kumrejesha kocha wake wa zamani Rafael Benitez (61) ambaye kwa sasa anainoa Everton (Football Insider).

Aliyekuwa kocha wa Roma Paulo Fonseca (48) anatarajia kupokea ofa ya kuwa Meneja mpya wa Newcastle, lakini wamiliki wapya wa klabu hiyo bado wanatafakari uamuzi wao (Fabrizio Romano, via Chronicle).

Barcelona bado ina matumaini ya kumpata kocha wa Liverpool Mjerumani Jurgen Klopp (54) kuchukua nafasi ya kocha wa sasa Ronald Koeman (Sport – in Spanish).

        > Tetesi za Soka Ulaya  Oktoba 26, 2021

Klabu ya Chelsea imepewa ofa ya kumsajili beki wa Uholanzi Matthijs de Ligt (22) wakati huu Juventus ikitaka kupunguza kiwango cha mishahara inayotoa kwa wachezaji (Goal – Star).

Arsenal inajiandaa kupambana na Manchester City katika mbio za kumsajili beki, Sergi Roberto (29) kama mchezaji huru kutoka Barcelona (Fichajes, talkSPORT).

Kiungo wa Manchester United Donny van de Beek (24) amemkataa wakala wa soka Mino Raiola baada ya wakala huyo kumuomba mholanzi huyo awe wakala wake mpya (Mike Verweij, via Express).

Klabu za Aston Villa, AC Milan na Bayer Leverkusen ni miongoni mwa vilabu vinavyomtaka mshambuliaji wa River Plate Julian Alvarez, 21 (CalcioMercato – Italian).

error: Content is protected !!