Rais Samia kuongoza baraza la biashara

HomeKitaifa

Rais Samia kuongoza baraza la biashara

Rais Samia Suluhu Hassan kesho anatarajiwa kuongoza Mkutano wa 14 wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) utakaofanyika Ikulu ya Magogoni, Dar es Salaam.

Katibu Mtendaji wa TNBC, Dk Godwill Wanga aliwaambia waandishi wa habari kuwa maandalizi ya mkutano huo yameshakamilika na wajumbe wa mkutano huo wamewasili Dar es Salaam. “Kaulimbiu ya mkutano huu ni ‘Mazingira Bora ya Biashara kwa Uchumi Himilivu na Shirikishi’,” alisema Dk Wanga.

Alisema moja ya mambo yatakayojadiliwa ni kupitia utekelezaji wa Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara (MKUMBI) nchini, ambao wajumbe watapata fursa ya kujadili mafanikio, changamoto na mapendekezo ya maboresho ya utekelezaji wake.

error: Content is protected !!