CCM kubadili katiba Aprili 1, 2022

HomeKitaifa

CCM kubadili katiba Aprili 1, 2022

Katibu Mwenezi CCM, Shaka Hamdu Shaka, leo Jumamosi, amesema Aprili 1, 2022,  chama hicho kitafanya mkutano mkuu maalumu kwa ajili ya kufanya marekebisho ya katiba yake ya 1977 , kwa lengo la kujiimarisha na kufanya marekebisho katika maeneo ambayo hakijafanya vizuri.

Shaka alisema lengo la marekebisha ni kupata viongozi imara, kukiimarisha chama na kuongeza kasi na ufanisi wa chama.

“Namba moja ni kuongeza kasi na ufanisi wa kazi za chama na utekelezaji wa maamuzi ya vikao, namba mbili kukiwezesha Chama Cha Mapinduzi kupata viongozi imara, waadilifu, wenye uwezo mkubwa wa kuongoza na kusimamia majukumu ya serikali za mitaa kwa ufanisi,”

“Namba tatu kuongeza na kuimarisha uthibiti wa chama kwa viongozi wake wanaochaguliwa kuongoza na kusimamia utekelezaji wa ilani ya CCM kupitia serikali za mitaa, namba nne kuimarisha nguvu ya chama katika kukabiliana na kuthibiti vitendo vya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka na namba tano kuongeza kuongeza uwakilishi wa jumuiya za CCM ngazi ya kata kwenye mkutano mkuu wa CCM wa wilaya na kurekebisha itifaki ya uwakilishi unaofanana na wenyeviti na makatibu wa jumuiya za CCM wa ngazi za mkoa kuwa wajumbe wa mkutano mkuu wa taifa na ngazi ya wilaya kuwa wajumbe wa mkutano mkuu wa mkoa,” alisema Shaka.

Aidha, Shaka pia alisema Kamati kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa imeielekeza Serikali kuangalia upya mwenendo wa jeshi la polisi nchini ambao umekuwa ukilalamikiwa na wananchi kutokana na matendo yanayofanywa kinyume na miongozo ya utendaji wa kazi.

 

error: Content is protected !!