CHADEMA yaainisha mafanikio ya ‘Join the chain’

HomeKitaifa

CHADEMA yaainisha mafanikio ya ‘Join the chain’

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Benson Kigaila ameeleza mafanikio ya programu yao ya Join the chain na kusema kwamba imesaidia chama kujitegemea kimapato na kujiendeleza bila kupokea ruzuku kutoka serikalini.

Hivi karibuni, Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe alionekana mara kadhaa akizunguka na kuzungumza na wanachama wao katika maeneo mbalimbali nchini akichangisha na kupokea michango kutoka kwa wananchi huku akieleza kuwa chama hicho kitaendeshwa na wananchi.

Kigaila alisema programu hiyo ina malengo makuu mawili ikiwamo kuwafanya Watanzania waungane katika suala la kudai katiba mpya na kukitengenza chama kimapato, jambo ambalo alidai kuwa limefanikiwa kwa kiasi kukibwa.

“Taasisi sustainable (endelevu) lazima iwe na uwezo wa kupata mapato kutoka ndani yake bila kutegemea wafadhili au hisani ya serikali na imefanikiwa ndiyo maana CHADEMA leo ipo haichukui ruzuku, lakini inafanya shughuli zote kama kawaida,” alisema Kigaila.

Aidha, Kigaila alisema kwamba baraza kuu la chama hicho linatarajia kukaa Mei 11, mwaka huu na ajenda moja wapo zitakazo jadiliwa itakuwa ni rufani ya wabunge wa viti maalumu wa chama hicho Halima Mdee na wenzake 18 na kufanya maamuzi. 

error: Content is protected !!