Ndugai kuacha siasa

HomeKitaifa

Ndugai kuacha siasa

Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai ametangaza nia yake ya kuacha siasa ikiwamo kutogombea tena nafasi ya ubunge katika jimbo la Kongwa mkoani Dodoma.

Alibainisha hayo Mei 8,2022 alipokuwa akizungumza kwenye ibada ya kuweka wakfu gari ya Pareshi ya Mtakatifu Michael Kanisa la Aglikana Tanzania Dayosisi ya Mpwapwa.

“2025 sitagombea nafasi ya ubunge tena nastaafu sio kama nastaafu kwa kushindwa, lakini ni jambo ambalo tayari nilishapanga kutoka muda mrefu uliopita hivyo tutaendelea kushirikiana kama ambavyo tunashirikiana sasa,” alisema Mbunge Ndugai.

Huu utakua uamuzi wa pili kuchukuliwa na kiongozi huyo baada ya kujiuzulu uspika hivi karibuni nafasi iliyochukuliwa na Tulia Ackson.

 

error: Content is protected !!