Sonona inavyoathiri wanawake kiakili

HomeKitaifa

Sonona inavyoathiri wanawake kiakili

Watu milioni nchini wanaishi na ugonjwa wa sonona huku wengi wao wakiwa wanawake.

Kauli hiyo imetolewa jana Dar es Salaam na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, wakati wa Kongamano la Kwanza la Kitaifa la Afya ya Akili huku akisema miongoni mwa dalili hatari za sonona ni kutosema changamoto zako kwa watu.

“Lakini hapa nahitaji pia tufanye takwimu kwa sababu tunaambiwa moja ya dalili ya hatari ya sonona ni kutosema changamoto zako kwa watu. Na wanawake tumekuwa wepesi kushirikisha watu changamoto zetu, kwa hiyo tunapoambiwa kwamba wanawake ndiyo tunaongoza ni vyema tutizame ni watu wapi zaidi wanaathirika na hili,” alisema Waziri Ummy.

Alisema Tanzania inakadiriwa kuwa na watu milioni saba wenye magonjwa mbalimbali ya akili, ikiwamo yanayotokana na matumizi ya dawa za kulevya, magonjwa ya akili mengi yaliyoko nchini ni yatokanayo na sonona, kihoro, sikozoflenia, matumizi ya bangi na pombe kupita kiasi.

“Na kuna uhusiano mkubwa na wa karibu wa uchumi katika ngazi ya mtu mmoja, familia, jamii na taifa kwa ujumla. Yapo magonjwa ya akili ambayo yanaathiri katika kufikiri, kuhisi, kutambua na kutenda na hivyo kuwa na mabadiliko ya kitabia na mwenendo ulio tofauti au usioendana na jamii husika, kiimani , kimila, kidesturi na nyanja nyingine za jamii,” alisema Waziri Ummy.

Waziri huyo wa Afya alisema ni muhimu Bima ya Afya ikakubali kugharamia wenye Afya ya akili ili kuwasaidia kupata matibabu kwa urahisi.

 

error: Content is protected !!