Padri amnajisi mtoto wakati akiungama

HomeKitaifa

Padri amnajisi mtoto wakati akiungama

Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi imeelezwa namna Paroko wa Parokia Teule ya Mtakatifu Dionis Aropagita  ya Jimbo Katoliki la Moshi, Padri Sosthenes Bahati (41) anavyodaiwa kumnajisi mtoto wa miaka 12 akiungama.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi, Salome Mshasha, wakili wa serikali, Kassim Nasri alidai mshitakiwa alitenda kosa hilo Agosti 12 mwaka huu akiwa ofisini kwake.

Ilidaiwa mahakamani hapo kwamba siku ya tukio mtoto huyo alikwenda katika Kanisa Katoliki Mtakatifu Dionis Aropagita lililopo eneo la Kawawa kwa lengo la kushiriki mafundisho ya Kipaimara.

Wakili Nasri alida kuwa jioni ya siku hiyo mtoto huyo alirudi kanisani hapo kuungama dhambi na alimkuta mshitakiwa akiwa amekaa katika kiti, akapiga magoti mbele ya kiongozi huyo wa kanisa ili kuungama.

Alidai wakati mtoto huyo akiungama mshitakiwa alimshika mabega na kisha kumpapasa mwilini, kifuani na sehemu za siri.

Wakili Nasri alidai kuwa baada ya kumpapasa alimuegemeza ukutani na kunyanyua sketi ya mtoto huyo na akamtaka aishilie na kisha akamshusha nguo za ndani.

Alidai kuwa mshatikwa alipandisha kanzu na akafungua suruali, akamnajisi mtoto huyo.

Wakili Nasri alieleza mahakama kwamba mtoto huyo alimweleza mama yake na uchunguzi ulipofanyika ilibainika mtoto huyo alinajisiwa.

 

error: Content is protected !!