Waliovujisha mitihani ya uuguzi kukiona

HomeKitaifa

Waliovujisha mitihani ya uuguzi kukiona

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dk Dorothy Gwajima amewataka watanzania kuwa na subira wakati uchunguzi ukiendelea kuhusu tuhuma za kuvuja kwa mitihani wa wauguzi ngazi ya Stashahada ili kubaini ukweli wa jambo hilo.

“Tume tuliyoiunda ipo mbioni kukamilisha uchunguzi wake na hivi karibuni itanikabidhi, na nataka niwahakikishie Watanzania, wale waliohusika kwa sababu wao wametuongezea  kazi zisizostahili na sisi serikali tutawaongezea kazi inayostahili kwa mujibu wa sheria kwa sababu ripoti ya awali inaonesha kuna uzembe,” alisema.

Dk Gwajima amesema tume aliyoiunda inatarijia kutoa taarifa yake Jumatatu wiki ijayo, aliyasema hayo wakati akizindua majengo ya Kituo cha Elimu ya Masafa Morogoro (CDE).

error: Content is protected !!