Tetesi za Soka Ulaya leo Oktoba 26 (Ole Gunnar njia panda Man United, huku Christensen na Chelsea mambo bado)

HomeMichezo

Tetesi za Soka Ulaya leo Oktoba 26 (Ole Gunnar njia panda Man United, huku Christensen na Chelsea mambo bado)

Uongozi wa Manchester United unafikiria kumtimua Solskjaer kabla ya mechi ijayo Jumamosi ugenini dhidi ya Tottenham (Manchester Evening News)

Zinedine Zidane (49) hafikirii kuwania kazi Old Trafford licha ya kutokua na timu tangu aondoke Madrid mwezi Mei.
Kiungo aliyewahi kuichezea Real Madrid anaelekeza macho yake kukinoa kikosi cha Paris St-Germain au timu ya taifa ya Ufaransa, ingawa kwa sasa timu hizo zina walimu hakuna nafasi (Mundo Deportivo – Spanish)

Newcastle United inamtaka kiungo wa Aston Villa na Zimbabwe Marvelous Nakamba 27, katika dirisha la Januari (Football Insider).

 > Zifahamu rekodi 6 za Manchester United zilizovunjwa na Liverpool ligi kuu ya England

Ryan Taylor (37) aliyekuwa beki wa Newcastle anasema Newcastle “Magpies” inapaswa kuzungumza na meneja wa Rangers Steven Gerrard (41) kuchukua mikoba ya kuwanoa matajiri hao wa St James’ Park (Sky Sports)

Mazungumzo ya mkataba mpya kati ya Chelsea na beki wa kati Andreas Christensen yamekwama kutokana na kutokuwepo kwa mawasiliano kwa miezi miwili baina ya pande hizo kuhusu mkataba mpya (Goal).

Beki wa Chelsea Trevoh Chalobah (22) anakaribia kusaini mkataba mpya wa muda mrefu baada ya kufanikiwa kuwa katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo (Football London).

Meneja wa Barcelona Ronald Koeman (58) ataweka kibarua chake matatani kama kikosi hicho kitashindwa kupata ushindi katika michezo mitatu ijayo (Marca).

Donny van de Beek (24) ameamua kubadili wakala wake akihaha kuondoka Manchester United mwezi Januari huku Everton, Newcastle na Juventus zikionyesha nia ya kumtaka kiungo huyo (Metro)

error: Content is protected !!