Bodaboda walalamika kuchapwa bakora na polisi

HomeKitaifa

Bodaboda walalamika kuchapwa bakora na polisi

Madereva wa pikipiki maarufu kama bodaboda wamemlalamikia Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Makongoro Nyerere kuwa polisi wamekuwa  wakiwachapa bakora bila kujua makosa waliofanya.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Babati, Abdulrahaman Kokoli  amekiri mbele ya Mkuu wa mkoa kuwa ni kweli vitendo hivyo vinafanywa na Polisi.

Mkuu wa mkoa amesema “Mimi sipendi watu wanyonge kuonewa wote tulioajiriwa na serikali hatutakiwi kupiga raia wa Tanzania kiboko, anaefanya hivyo anakosea hata kama ni askari polisi anavunja sheria ya Tanzania, lakini pamoja na upungufu huo sitakubaliana na vitendo vyovyote vya kikatili vinavyofanywa na askari yoyote wa jeshi la polisi.”

error: Content is protected !!