Ujumbe uliotumwa na wafungwa waliohukumiwa kunyongwa kwenda kwa Rais Samia

HomeKitaifa

Ujumbe uliotumwa na wafungwa waliohukumiwa kunyongwa kwenda kwa Rais Samia

Wafungwa waliopo gereza la Uyui mkoani Tabora wametuma salamu kwa Rais Samia Suluhu Hassan kupitia risala iliyosomwa na mfungwa kiongozi, Masali Misalaba mbele ya makatibu wakuu watatu wa Wizara ya Katiba na Sheria wakiongozwa na katibu mkuu, Profesa Sifuni Mchome.
 
“Sisi wafungwa tuliohukumiwa kunyongwa, tunaomba utufikishie ombi letu kwa Rais Samia atuonee huruma na atupunguzie adhabu ili nasi tuweze kufanya kazi. Tuna wakati mgumu na tunawasumbua askari magereza,” amesema Misalaba.
Mahabusu na wafungwa wengine nao waliiomba serikali kuangalia upya utaratibu wa msamaha wa wafungwa unaotolewa na Rais.
 
Aidha, Katibu Mkuu, Profesa Machome amewajibu wafungwa hao na kuwaambia kwamba atafikisha ombi hilo kwenye mamlaka zinazohusika.
error: Content is protected !!