Leo katika historia: Hosni Mubarak anachaguliwa kuwa Rais wa Misri

HomeElimu

Leo katika historia: Hosni Mubarak anachaguliwa kuwa Rais wa Misri

Tarehe na siku kama ya leo mwaka 1981, Makamu wa Rais wa Misri, Hosni Mubarak anachaguliwa kuwa Rais wa nchi hiyo baada ya Rais Anwar Sadat kuuawa. Mubarak aliondolewa madarakani mwaka 2011 kwa shinikizo la wananchi.

Mubarak alijiunga na Chuo cha Kijeshi cha Misri, ambapo alipata Shahada ya kwanza ya Sayansi ya Kijeshi mnamo Februari, 1949 na kuhitimu kama Luteni. Kisha, akajiunga na Chuo cha Jeshi la Anga na alipata Shahada ya Sayansi ya Anga, Machi 12, 1950.

    >Leo katika historia: Eliud Kipchoge anaweka rekodi ya kukimbia marathon chini ya saa mbili

Akapandishwa cheo katika vituo vya Jeshi na kuwa Mhadhiri katika Chuo cha Jeshi la Anga, na kuwa mkufunzi Mkuu Msaidizi wa Chuo hicho, kisha Mkuu wa Wafanyakazi na Kamanda wa Kikosi wakati huo huo hadi 1959.

error: Content is protected !!