Serikali kuajiri wahandisi 260

HomeKitaifa

Serikali kuajiri wahandisi 260

Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mohamed Mchengerwa ameeleza serikali imetoa kibali cha kuajiri wahandisi 260 ambao watapelekwa kwenye Halmashauri ili kusimamia kikamilifu miradi ya maendeleo inayotarajia kuanza kutekelezwa hivi karibuni kutokana na fedha nyingi zilizotolewa na Rais Samia Suluhu

Pamoja na hayo Waziri Mchengerwa ameeleza kuwa Serikali inatarajia kuongeza idadi ya watumishi wanaopaswa kupandishwa madaraja kwa mwaka wa fedha 2021/2022 kutoka watumishi 90,000 hadi kufikia watumishi 180,00, na kuwataka maofisa utumishi kutumia fursa hiyo kuhakikisha inawapandisha watumishi kwa kuzingatia sifa na vigezo na waajiri wametakiwa kuweka bajeti ya upandishaji vyeo kwa mwaka wa fedha ujao.

    > Ujumbe uliotumwa na wafungwa waliohukumiwa kunyongwa kwenda kwa Rais Samia

Akizungumzia madai ya watumishi, Waziri Mchengerwa amewataka waajiri kuingiza madai ya malimbikizo ya mishahara katika mfumo wa bajeti na kuhakikisha kuwa maofisa utumishi wanafanya vikao kwa kuwatembelea katika maeneo ya kazi na kusikiliza kero za wafanyakazi. #clickhabari

error: Content is protected !!