Matumaini kero za muungano

HomeKitaifa

Matumaini kero za muungano

Huku leo Aprili 26, 2022 Tanzania ikisherehekea Muungano wa Tanzania unaoundwa na Tanganyika na zanzibar, kero 18 kati ya 25 zimetatuliwa.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Selemani Jafo ameeleza kuwa kwa kushirikiana na wixara pacha ya Zanzibar walifanikiwa kutatua changamoto saba kwa mwaka 2020 na kubakiwa na kero 18 kati ya kero 25.

“Lakini kwa uongozi wenu wewe [Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango] na mheshimiwa Rais [Samia Suluhu Hassan] tumefanikiwa kutatua kero 11 mwaka 2021 na hivyo ukijumlisha na zile saba zinakuwa 18,”amesema Dkt. Jafo .

Aidha, katika hafla hiyo ya Muungano ambayo Dkt. Mpango ndio mgeni rasmi, amezindua kitabu zheny kuuongelea Muungano kwa upana wake kwa manufaa ya wengi kizazi hiki na kijacho.

Dkt. Jafo amependekeza iliwezekana kitabu hicho kitumike katika kufundishia somo la historia.

Kutatuliwa kwa kero 18 za muungano kunafanya idadi ya kero zinazohitaji utatuzi kubakia saba.

 

 

error: Content is protected !!