Steve Nyerere aachia kiti

HomeBurudani

Steve Nyerere aachia kiti

Msanii Steve Nyerere ametangaza kujiuzulu kutoka nafasi ya usemaji wa Shirikisho la Muziki Tanzania (SMT) baada ya kuibuka kwa watu wasio na imani naye.

Steve amewaambia waandishi wa habari kuwa mbali na kujiuzulu ataendelea kutoa msaada kwa wanamuziki mbalimbali pale atakapohitajika kufanya hivyo akishirikiana na viongozi wa shirikisho akiwemo Mwenyekiti, Ado November.

“Nimeamua kuachia ngazi. Nimeamua kujiuzulu kutoka kwenye nafasi hii rasmi, niendelee na kazi nyingine za msingi,” amesema Steve.

Awali, hoja za kumkataa Steve Nyerere zilifikishwa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) nao kuahidi kufuatilia mgogoro huo kwani hoja za pande zote mbili zilikuwa na mashiko.

error: Content is protected !!