Netflix kuwekeza bilioni 146.2 Afrika Kusini

HomeBurudani

Netflix kuwekeza bilioni 146.2 Afrika Kusini

Netflix kuwekeza bilioni 146.2 Afrika KusiniMtandao wa sinema Netflix wamejipanga kuwekeza $63 m sawa na takribani randi milioni 900 nchini Afrika Kusini ili kukuza soko la filamu za Kiafrika.

Wakati wa Mkutano wa Nne wa Mwaka wa Uwekezaji Afrika Kusini Netflix wamesema jumla ya programu nne zitafanywa, tatu za wazawa na moja ya kimataifa.

“Netflix imejithabiti Afrika Kusini kwa muda mrefu na tunawekeza katika vipaji mbele na nyuma ya kamera,” alisema Shola Sanni, Mkurugenzi wa Netflix Sera ya Umma ukanda  wa Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Fedha zilizotolewa ni sawa na shilingi bilioni 146.2 za Kitanzania.

Wiki iliyopita, Machi 18, Tanzania ilipata uwakilishi katika series ya ‘Young, Famous and African’ iliyorekodiwa Afrika Kusini ambapo mwanamuziki Diamond Platnumz alikuwa miongoni mwa washiriki.

error: Content is protected !!