Insta yamfungia Kanye: apanga kuja na mtandao wake

HomeBurudani

Insta yamfungia Kanye: apanga kuja na mtandao wake

Kampuni ya Meta imemfungia rapa Kanye West “Ye” kutopost kwa saa 24 kuanzia jana Machi 16 baada ya rapa huyo kupost picha ya mchekeshaji Trevor Noah na kuandika ujumbe wenye maudhui ya ubaguzi wa rangi.

Kanye amemuita Trevor ‘Koon’ neno lenye kumaanisha mtu mweusi ambaye anapinga watu weusi na anatenda dhidi ya watu weusi. jambo ambalo ni kinyume na sheria za Meta.

Noah, Mwafrika Kusini anayefanya shughuli zake Marekani katika kipindi chake cha ‘The Daily Show’ alizungumzia sakata linaloendelea kati ya Ye, aliyekuwa mkewe Kim Kardashian na mpenzi mpya wa Kim, Pete Davidson na kusema kuwa Kanye sasa anahitaji msaada kwani anayoyafanya yanavuka mipaka na heshima kwa Kim.

“Kanye amekuwa mchokozi kwa namna anavyojaribu kumrudisha Kim. Alivyoanza, ilikuwa, unajua, wengine wangesema ya kimahaba.“Oh, bado nakuhitaji. Na, unajua, haya hapa maua,” alieleza Ye.

“…na baadhi ya watu walielewa. oo anajaribu kurudiana na mpenzi wake. “Tunaelewa hilo. Lakini baada ya muda, imekuwa na uhasama zaidi na zaidi.

Kufuatia sakata hilo, rafiki wa karibu wa Kanye, mwanamuziki French Montana ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter na kusema baada ya ye kufungiwa Instagram ameamua kuja kivingine.

“Instagram imemfungia kwa muda mshikaji wangu Kanye, anakaribia kutengeneza mtandao wake wa kijamii,” aliandika.

Je! Unadhani Kanye atafungua mtandao wa aina gani au ataupa jina gani?

error: Content is protected !!