Historia imeandikwa Kituo cha Afya Masasi

HomeKitaifa

Historia imeandikwa Kituo cha Afya Masasi

Kwa muda mrefu wananchi wa wilaya ya Masasi kata ya Chikundi wamekuwa wakiishi na changamoto kubwa ya upatikanaji wa huduma za afya katika maeneo ya karibu.

Iliwalazimu kwenda mbali na kutumia gharama kubwa na kupelekeawakati mwingine wajawazito kupoteza maisha.

Moza Kaspari ni mmoja wa wahanga wa changamoto hiyo lakini sasa anamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kujenga kituo cha afya cha kata hiyo na kukiri kwamba sasa hawatapata tena shida na wajawazito watajifungua salama.

“Ukiwa na ujauzito, kwenda Ndanda lazima ukodi gari ambalo ni shilingi elfu kumi na ukichukua bajaji ni shilingi elfu sita. Kwa kipindi chote tumekuwa tukiishi maisha hayo ya shida na ukifika kule gharama za matitabu ni kubwa sana kiasi kwamba watu wengine wanazalia nyumbani na kupoteza watoto.

“Nina mshukuru Mama Samia , yani shukurani zangu ni za dhati na sio mimi tu, wananchi wote wa tarafa hii na kata hii wanashukuru sana. Mimi kama mama nasema kweli mama yeyote akiwa kiongozi anakuwa na huruma na anaokoa maisha ya watu, sio ya mtu mmoja, jamii yote. Mimi naamini hata na wapita njia watakuja kutibiwa hapa,” alisema Moza.

error: Content is protected !!