Zijue sababu 3 kwanini utumie maji ya Malimao kwenye sura yako

HomeElimu

Zijue sababu 3 kwanini utumie maji ya Malimao kwenye sura yako

Limao ni tunda jamii ya Chungwa ambalo hutumika sana kama kiungo kwenye chakula. Licha ya matumizi ya limao katika maisha yetu ya kila siku, lakini bado uelewa juu ya faida za tunda hili umekuwa mdogo miongoni mwa walio wengi.

Limao lina faida sana katika kutunza afya zetu, moja ya faida itokanayo na limao ni virutubisho vinavyosaidia kutunza ngozi.

Matabibu wa maswala ya tiba asilia wanasema kuwa matumizi ya limao kwa minajili ya kutunza ngozi yanaweza kutekelezwa kwa namna tofauti. Moja, ikiwa ni kutumia kama kinywaji, na pili unaweza kutumia kwa kupaka kwenye ngozi.

Limao lina utajiri wa Vitamini C na virutubisho vingine kama ‘Vitamini A’, ‘Vitamini E’, ‘Vitamini K’, madini ya ‘Calcium’, ‘Folate’, ‘Magnesium’, ‘Potassium’, ‘Choline’, ‘Phosphorus’ pamoja na ‘Betaine’.

 1. Maji ya limao huondoa madoa kwenye Ngozi
  Aina ya madini ya virutubisho vilivyotajwa hapo juu ni moja ya kemikali asilia kwenye limao ambazo zina kazi kubwa ya kung’arisha ngozi. Cha kufanya kamua maji ya limao kwenye kikombe au chombo kisafi, kisha chovya kwa pamba safi na kisha upakae maeneo yenye madoa, halafu acha ikauke kwa muda kwa dakika 30 halafu uoshe kwa maji masafi. Rudia utaratibu huo kwa mwezi mmoja, na inashauriwa kufanya hivyo usiku kabla ya kulala.

   > Zijue njia 7 za kuzuia kunyonyoka nywele kwa wanaume

 2. Maji ya limao huondoa chunusi na makunyazi
  Maji ya limao ni dawa nzuri sana kwa ngozi yenye chunusi na makunyazi. Limao linaweza kukupa matokeo mazuri kwenye kutibu ngozi yako ndani ya muda mfupi sana. Hapa unashauriwa kutumia limao na asali, chukua limao na kamulia maji yake kwenye chombo kisafi, kisha changanya na asali upate mchanganyiko uliochanganyika vizuri. Kisha paka usoni ukiwa tayari umeshauosha uso wako wa maji bila kutumia sabuni, na umekauka vizuri. Pakaza vizuri kisha acha ikauke kwa dakika 30, halafu osha kwa maji safi na upumzike ukiacha uso wako ukiwa mkavu kabisa. Tiba hii ni nzuri zaidi kwa watu wenye ngozi yenye asili ya mafuta.
 3. Limao hunyinyirisha Ngozi
  Kwa ngozi yenye kung’aa vyema, basi unahitaji maji ya limao, glasi moja ya maji yenye uvuguvugu pamoja na asali. Changanya vizuri kisha paka usoni kila siku asubuhi kwa kipindi cha mwezi mmoja. Hakikisha kuwa unatengeneza mchanganyiko ambao utaweza kutumia mara moja, kwa sababu mchanganyiko ambao umelala sio mzuri kwa ngozi yako. Tengeneza kiasi cha kutosha kwa matumizi ya mara moja tu.
error: Content is protected !!