Rais Samia aliwaza mbali nyongeza ya mishahara

HomeKitaifa

Rais Samia aliwaza mbali nyongeza ya mishahara

Mei 14,2022 , Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan alitimiza ahadi yake ya kuongeza mishahara kwa kutangaza kima cha chini kwa watumishi wa umma kupanda kwa asilimia 23.3.

Ongezeko hilo la mishahara ya watumishi wa umma lina manufaa kwa jamii ikiwa ni pamoja na kuchochea shughuli za kijamii na kiuchumi kwa sababu Rais Samia ametekeleza jambo ambalo halikufanyiwa kazi kwa takriban miaka saba.

Kutokana na ongezeko hilo, serikali imepanga kutumia kiasi cha Sh 9.7 trilioni katika mwaka wa fedha 2022/23 kwa ajili ya kugharamia malipo ya mishahara ya watumishi wa umma.

Faida za ongezeko la mishahara

Kuongeza mzunguko wa wa fedha

Ongezeko hilo litawafanya watumishi kuingiza fedha kwenye mzunguko wa uchumi ikiwa ni pamoja na kutoa michango kwenye harusi, kulipa ada za shule, kuwatumia ndugu fedha za matumizi, kujenga nyumba na kununua bidhaa au vifaa.

Jamii inapata fedha kupitia mzunguko wa wenzao wenye ajira. Kwa kuwa wao kama jamii hawana njia yoyote ya kupata hela kutoka katika mfuko wa serikali yaani hazina moja kwa moja.

Kuchochea ari ya kufanya kazi

Nyongeza hiyo inachochea ari ya kufanya kazi kwa watumishi kwani wana uhakika na kiasi cha fedha wanachopata.

Watumishi wanapofanya kazi kwa bidii uchumi unakua kwa sababu kutakua na ongezeko la uzalishaji wa bidhaa kutokana na nguvu iliyowekwa katika utendaji kazi.

Kuondoa msongo wa mawazo

Ongezeko hii imeleta faraja na kuondoa msongo wa mawazo kwa wafanyakazi wenyewe na hata familia zao. Kimsingi, ongezeko la mshahara limepunguza msongo wa mawazo na kuimarisha ndoa na hatimaye huondoa migogoro ya kifamilia na kudumisha mahusiano baina ya wanandoa, ndugu, watoto na hata wafanyakazi wenyewe kwa wenyewe.

Mtumishi sasa atakuwa hawazi tena madeni sababu ya ongezeko hilo la mshahara.

Aidha, ukweli lazima usemwe, ingawa gharama za maisha zimepanda na kuna mfumuko wa bidhaa kila pande ya dunia, Rais Samia Suluhu ameamua kuwapa unafuu wa maisha wananchi wake kwa kuongeza kima hicho cha mishahara, kutoa bilioni 100 kwa ajili ya kukidhi bei za mafuta kila mwezi na kupandisha vyeo watumishi wa umma.

 

error: Content is protected !!