Ngorongoro mambo safi

HomeKitaifa

Ngorongoro mambo safi

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Rais Samia Suluhu ametoa fedha kukamilisha mchakato wa wananchi kuhama kutoka Ngorongoro kwenda Kijiji cha Msomera wilayani Handeni na hadi juzi kaya 293 zilikuwa zimejiandikisha kukubali kuhama kwa hiari.

Majaliwa alisema bungeni Dodoma kuwa kaya hizo zina wakazi 1,497 walioandaliwa mazingira bora ya kuishi yakiwemo makazi.

“Tutapeleka malori kwa ajili ya samani na malori ya kubeba mifugo na tunawalipa fidia ya nyumba zao. Maandalizi yote haya Rais Samia Suluhu Hassan ameshatoa fedha, fedha tunayo sasa kazi iliyobaki ni kwenda kutekeleza,” alisema Majaliwa baada ya kipindi cha maswali na majibu.

Aidha, Waziri Majaliwa alisema serikali imejenga shule ya msingi yenye vyumba saba, imejenga sekondari yenye vyumba vinane na imekarabati zahanati itakayotibu wananchi katika Kijiji cha Msomera na Kijiji cha jirani.

 

error: Content is protected !!