Justin Bieber apooza uso

HomeKimataifa

Justin Bieber apooza uso

Msanii kutoka nchini Canada, Justin Bieber ameweka video fupi Kwenye ukurasa wake wa Instagram akieleza wazi kwamba amesitisha show zake kutokana na ugonjwa wa kupooza uso. 

“Habari Kila Mmoja…Justin Hapa !! ..kama Unavyouona uso wangu. Nina ugonjwa huu uitwao Ramsay Hunt syndrome na ni kutokana na virusi hivi ambavyo hushambulia mishipa ya fahamu katika sikio langu na mishipa yangu ya uso Ambayo Ndio Imepelekea uso wangu kupooza (Face Paralysis).”

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Justin Bieber (@justinbieber)

“Siwezi kuamini, Nimefanya kila kitu ili kupata nafuu lakini ugonjwa huu unazidi kuwa mbaya, Moyo wangu unaniuma kwamba nitalazimika kuahirisha tour yangu (maagizo ya madaktari). Kwa watu wangu wote nawapenda sana na nitapumzika na kupata nafuu……….

“Natamani isingekuwa hivyo lakini ni wazi mwili wangu unaniambia nipumzike, kama unavyoona jicho langu hili halipepesi, pua yangu haisogei upande huu wa uso haufanyi kazi mishipa yangu ya sikio pia”

 

error: Content is protected !!