Wenye visima ruksa kusambaza maji

HomeKitaifa

Wenye visima ruksa kusambaza maji

Wakati Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (Dawasa) ikitoa ratiba ya mgao wa maji, Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ametembelea eneo la matengenezo ya bomba kubwa la inch 72 katika kata ya Wazo, Jijini Dar es salaam ambalo ni sehemu ya kimkakati ya kuongeza msukumo wa Maji katika Jijini Dar es salaam .

Katika ziara hiyo, Aweso ameagiza kuruhusiwa kwa wenye visima binafsi kuhudumia wananchi.

Akitoa tamko hilo jana Oktoba 27, 2022 amesema serikali imeruhusu matumizi ya maji ya visima binafsi na vya umma ili vitumiwe na kuendelea kutoa huduma kwa wananchi bila kikwazo chochote hadi hapo itakapotangazwa vinginevyo.

“Wenye visima binafsi toeni huduma sasa ili wananchi wasiteseke na huduma hii.” Amesema.

Aidha, ameiagiza DAWASA kuhakikisha ratiba ya mgao wa maji inasimamiwa na kufuatwa kikamilifu kama ilivyopangwa.

error: Content is protected !!