Vijana 812 wachaguliwa kujiunga programu ya kilimo

HomeKitaifa

Vijana 812 wachaguliwa kujiunga programu ya kilimo

Vijana 812 wamechaguliwa kujiunga na mafunzo maalumu ya Kilimo yanayoratibiwa na Wizara ya Kilimo.

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe ametangaza majina ya waliochaguliwa kwa awamu ya kwanza ya mafunzo hayo yajulikanayo kama Building a Better Tomorrow (BBT).

Takwimu zinaonesha kuwa kati ya vijana waliochaguliwa wanaume wameongoza idadi hiyo wakiwa ni 530 sawa na asilimia 65 huku wanawake ni 282 sawa na asilimia 35.

Bashe amefafanua idadi ya walioomba kujiunga na mafunzo hayo ni 20,227 ambapo mkoa wa Dar es Salaam umeongoza kwa kuwa na waombaji 2,931 huku Lindi ikiwa ya mwisho kwa kuwa na idadi ya vijana 109 waliotuma maombi hayo.

Vijana hao wanahitajika kuripoti katika vituo walivyopangiwa machi 17 mwaka huu ili kuanza mafunzo ya miezi minne kabla ya kukabidhiwa mashamba yao.

 

error: Content is protected !!